Swahili News

Hans van der Pluijm; Nitaifanya Azam FC icheze mchezo wa kuvutia na kutwaa mataji

KATIKA umri wa miaka 69 sasa, golikipa wa zamani na mchezaji wa FC Den Bosch na timu ya Taifa ya Holland, Hans van der Pluijm amechukua kazi mpya ya kukinoa kikosi cha Azam FC ya Dar es Salaam, Tanzania.

Kocha huyo wa zamani wa Excelsior ( 1995-1996), Obuasi Goldfields ( 2000-2002), Heart of Hoak ( 2002-2003), Ashanti Gold Sports ( 2004-2005) amewahi kushinda mataji mawili ya ligi kuu Tanzania Bara akiwa na kikosi cha Yanga SC misimu ya 2014/15 na 2015/16 sambamba na mataji ya Azam Sports Federations ( FA Cup) mwaka 2016 na Ngao ya Jamii 2015, alikuwa na msimu mmoja wa kupendeza kiasi wakati akiifundisha Singida United msimu uliopita.

Hans hakuogopa kuchukua nafasi ya kuionoa Singida United ambayo ilikuwa katika ligi ya chini kwa miaka 15 mfululizo na aliweza kuisaidia kufika fainali ya FA msimu uliopita ambayo walipoteza 3-2 mbele ya Mtibwa Sugar FC.

Kocha huyo aliweza kuupendezesha mchezo wa Yanga kwa miezi yote 30 aliyofanya kazi na mabingwa hao mara 27 wa kihistoria Tanzania Bara, mchezo wake wa kuvutia pia ulendelea katika miezi yake 12 akiwa Singida na hilo limechangia kwa kiasi kikubwa matajiri wa Azam FC kumtupia jicho na kumsaini.

Amepokea timu change katika soka la Tanzania ( miaka kumi) lakini tayati timu hiyo ina taji moja la ligi kuu Tanzania Bara ambalo walishinda pasipo kupoteza mchezo msimu wa 2013/14. Na hivi karibuni ikiwa chini yake na msaidizi wake Juma Mwambusi wameweza kuiongoza timu hiyo kutwaa taji lake la pili kihistoria la michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati-Cecafa Kagame Cup baada ya awali kushinda kwa mara ya kwanza mwaka 2015.

Hii inamaanisha kuwa kazi yake ya sasa imeanza vizuri na ni yeye ( Hans) ambaye anaweza kuisaidia klabu hiyo tajiri kurejea katika ushindani baada ya misimu miwili isiyovutia licha ya kusainiwa kwa wachezaji wengi wa Kimataifa.

www.sokafrika.com kupitia mwakilishi wake wa Tanzania ( Baraka Mbolembole) imefanya mahojiano ya kocha Hans van der Pluijm na hapa tunakuletea sehemu ya mahojiano hayo.

www.sokafrika.com: Baada ya vipindi viwili tofauti kama kocha wa Yanga na makombe mawili ya ligi kuu, moja Ngao ya Jamii na lingine moja la FA, mwaka wako mmoja Singida United ambako ulifanikiwa kuifikisha fainali ya FA msimu uliopita, kazi yako ya sasa Azam FC inamaana gani?

HANS VAN DER PLUIJM:

“ Kuanza kazi mpya hapa ni kuchukua jukumu Azam FC, inamaana hii ni changamoto mpya.Lengo langu na timu Kwa ujumla ni kuleta changamoto katika ligi kuu na kombe la Azam. Kila mwaka ligi inaongeza ushindani hivyo itakuwa ngumu. Tunatambua tunatakiwa kujiandaa kwa hilo kimwili, kiufundi na kimbinu.”

“ Tunahitajika kuwa na ukomavu kiakili katika mechi za nyumbani lakini zaidi ni katika mechi za ugenini.Tutatakiwa kucheza mechi zote kama fainali hivyo ndivyo wapinzani watakavyocheza dhidi ya Azam pia.Inahitaji ukomavu wa hali ya juu kwa kila mchezaji kuendana na hilo.”

“ Sitoacha hata kidogo falsafa yangu ya mpira. Mpira unatakiwa kuchezwa na kufurahiwa na wachezaji na kuleta furaha kwa mashabiki. Tutajaribu kuwavutia mashabiki, kuwa na nidhamu na kuwa bora zaidi katika soka ya kushambulia na kutengeneza timu yenye roho ya Ushindi ndani yake.”

www.sokafrika.com: Tayari umeshinda Cecafa Cup, je tutaraji nini kutoka kwa Azam msimu ujao wa ligi hasa ukizingatia hawakuwa na misimu miwili ya kuvutia?

HANS VAN DER PLUIJM:

“ Kitu muhimu ni timu kujiamini na kuendana na mchezo mzuri unaovutia wa kushambulia ambao ni muhimu kwa timu kupata matokeo mazuri. Tutaifanya hiyo mechi kwa mechi na tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kupata utendaji ulio bora kutoka kwa kila mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla.”

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

Simply football news!

There is football and there is the HEAVY DETAILED NEWS on the Sport where we give the news ,reviews ,analysis, statistics and live coverage of all the soccer events in Africa. We are Africa’s number one online soccer community created by true fans.

Copyright © 2018 Sokafrika.com. All rights reserverd.

To Top
WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com