Swahili News

Himid Mao; Baada ya michezo miwili katika jezi ya Petrojet, afunguka kwanini alikwama Denmark

BAADA ya misimu nane iliyoambatana na mataji ya Cecafa Kagame Cup, ligi kuu Tanzania Bara na Ngao ya Jamii mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati, Himid Mao Mkami ‘Ninja’ ameanza vyema maisha yake ya soka la kulipwa katika klabu ya Petrojet ya ligi kuu Misri.

Namshukuru Mungu na naishukuru Azam FC kwa kuniamini tangu nikiwa mdogo na kuniamini. Haikuwa rahisi, lakini wao waliniamini na nitaendelea kuiheshimu klabu hiyo pamoja na wachezaji wote niliopata kucheza nao kwa kipindi cha miaka yote nane.” Anaanza kusema Himid na kuongeza.

“ Kuwa sehemu ya mafanikio yote ya klabu nikiwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kwa muda mrefu katika klabu ambayo imewahi kusaini wachezaji wengi wazuri msimu kwa msimu kwangu ni kumbukumbu nzuri sana.nimewea kuweka alama na kutetea nafasi yangu kila siku,”

Himid, 26, alianza sambamba na Ahmed El Agoze katika nafasi ya kiungo wakati timu yake ilipolazimishwa suluhu-tasa dhidi ya Zamalek SC wikendi iliyopita na Jumatatu hii wawili hao walianza tena kwa pamoja katika mchezo wa 0-0 ugenini dhidi ya vigogo wengne katika soka la Misri Ismailia SC.

“ Ni matokeo mazuri sana kwetu.” anasema mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania wakati alipofanya mahojiano na mwandishi wa www.sokafrika.com ( Baraka Mbolembole). “ Tumeanza msimu dhidi ya timu kubwa katika ligi ya Misri, mashabiki na watu wote wa klabu wamefurahishwa na kiwango chetu. Sasa tunasubiri mechi ijayo ugenini dhidi ya Wedi Degla Februari 10.”

Himid alianza kucheza soka la ushindani mwaka 2010 akitokea timu ya vijana ya Azam FC na alikuwa sehemu ya wachezaji muhimu wakati klabu hiyo ilianzishwa miaka kumi iliyopita iliposhinda ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara msdimu wa 2013/14, pia alikuwa mchezaji ‘asiyegusika’ wakati Azam FC iliposhinda taji lake la kwanza la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati- Cecafa Kagame Cup mwaka 2015.

Sijapata shida sana kiuchezaji katika michezo miwili ya mwanzo hii inatokana na mimi kuwepo sehemu yote ya maandalizi ya msimu jambo ambalo limenisaidia kuzoea hali ya mpira wa hapa ( Misri). Nilipata tabu kwenye mechi ya maandalizi dhidi ya Ismaili na Jumatatu hii nilienda kucheza dhidi yao katika ligi nikiwa tayari nafahamu mambo muhimu kuhusu wao. Ilinisaidia sana.” Anasema motto huyo wa mwanasoka nyota wa zamani wa Tanzania, Mao Mkami.

“ Kiuchezaji kuna tofauti kubwa kati ya mpira wa nchi za ukanda huu wa Kaskazini na kwetu Afrika Mashariki. Wenzetu wanatumia kasi sana, nguvu na ufundi. Kikubwa wachezaji wanacheza kwa asilimia kubwa kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kwa asilimia kubwa tofauti na kwetu. Kwa kifupi, wanatumia vitu vyote, nguvu, kasi, na akili lakini kwenye maeneo na wakati mwafaka.”

“ Najisikia vizuri na huru kuwa hapa ( Petrojet) na kusema kweli nilihitaji changamoto mpya kwa muda mrefu. Kwa miaka takribani mitatu nilihitaji kucheza nje ya Tanzania na huu ndio muda ambao Mungu ameona ni sahihi.” Anaongeza kusema mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza pia kama mlinzi wa pembeni.

Mwaka mmoja uliopita Himid alikwenda kufanya majaribio katika timu ya ligi kuu Denmark ya Randers na licha ya kusemwa kuwa alifanikiwa kufuzu katika majaribio hayo lakini mchezaji huyo alirejea Tanzania na kuendelea kuichezea Azam FC. Akizungumza na sokafrika.com kiungo huyo ameweka wazi kwa mara ya kwana ni kwanini hakujiunga na Randers.

“ Nilienda katika majaribio Renders mwaka jana wakati huo nikiwa mchezaji wa Azam FC, lakini wakala wangu aliwaambia naenda kama mchezaji huru na kusaini mkataba. Baadae kuna mtu wa Azam alituma email kuwaambia mimi ni mchezaji wa Azam na baada ya majaribio natakiwa kurudi Azam kujadili kuhusu uhamisho. “

“ Lilikuwa ni jambo lililowashangaza Randers, lakini makubaliano yangu na wakala ilikuwa tutoe kiasi cha pesa yangu tuilipe Azam lakini tayari Randers waliona tumefanya udanganyifu, wakasema watakuja Tanzania kuongea na Azam lakini hawakuwahi kuja na kila ktu kiliishia hapo.”

Akiwa sasa ametimiza ndoto yake ya kucheza mpira wa kulipwa nje ya Tanzania, Himid ameichagua ligi kuu ya Misri na katika michezo yake miwili ya mwanzo ameshuhudia viwanja vyote ( nyumbani na ugenini) kukiwa na watazamaji wachache majukwaani.

“ Tangu zilipotokea vurugu na watu kufa kwenye mechi ya Al Masri na Al Ahly miaka ya karibuni mamlaka za Kiserikali zimeruhusu asilia kumi tu ya mashabiki kuhudhulia viwanjani. Kazi yangu ni kucheza mpira, uwepo wa mashabiki ama kutokuwepo si jambo nalotazama, natakiwa kutimiza majukumu yangu kwa asilimia zote.”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

Simply football news!

There is football and there is the HEAVY DETAILED NEWS on the Sport where we give the news ,reviews ,analysis, statistics and live coverage of all the soccer events in Africa. We are Africa’s number one online soccer community created by true fans.

Copyright © 2018 Sokafrika.com. All rights reserverd.

To Top
WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com