Wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania ‘TAIFA STARS’ wako safarini kuelekea nchini Uganda tayari kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Afcon.
Mchezo huo dhidi ya Uganda unatarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 8 nchini Kampala, Uganda.
Wakati huo huo Beki wa Kati wa Yanga Sc na Taifa Stars Kelvin Yondan atashindwa kuungana na kikosi hicho Uganda sababu ya Majeraha.Kwa mujibu wa Daktari wa timu ya Taifa ameshauri mchezaji huyo apumzike hivyo hatoshiriki mchezo huo dhidi ya Uganda.
Mashabiki wa Taifa stars na Yanga Sc wana maoni tofauti juu ya Yondan kutokua katika kikosi hicho dhini ya Uganda Jumamosi hii wakitambua mchango wake katika kuipa timu yao ushindi.
Je nani ataibuka mshindi katika mechi hiyo ya Taifa ya Tanzania na Uganda? Ambapo Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikua julai 4 mwaka 2015 ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1:1
